Ahukumiwa Miaka 5 Kwa Kusambaza Corona



Raia mmoja wa #Vietnam, Le Van Tri, amehukumiwa kifungo cha miaka mitano na faini ya Dola 880 (Takriban Tsh. Milioni 2) kwa kukiuka masharti ya #COVID19 na kusambaza Ugonjwa kwa watu 8 ambapo mmoja amefariki dunia

Mwanzoni mwa Julai, mshtakiwa alisafiri kwa kutumia pikipiki kutoka Mji wa Ho Chi Minh mpaka Ca Mau, ikielezwa alidanganya kuhusu hali yake kiafya na kusambaza Virusi kwa Wanafamilia na Wafanyakazi wa Kituo cha Ustawi alichotembelea

Mbali na kuweka masharti makali maambukizi yamekuwa yakiongezeka kwa kasi Nchini humo tangu mwezi Juni baada ya kuibuka Kirusi cha #Delta

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad