Ali Kamwe "Simba Waliuza CHAMA wakanunua MABASI, Mambo 10 Nilioyaona Simba vs Yanga"


Mambo 10 nilioyaona Simba vs Yanga

1: DAR ES SALAAM is Green and Yellow🟢🟡 YEES! CHAMPIONS wamerudi na Taji la kwanza la Msimu 🏆 Kuna Raha kubeba NGAO Lakini kuna Raha kubeba NGAO mbele ya Mtani wako👏

2: Ile Pacha ya AUCHO na BANGALA ni ndoto iliyokuwa ikiishi kwenye njozi za mashabiki wa Yanga🙌 Wagumu, wakatili wenye akili kubwa kichwani. Plan ya Gomes ilifia hapa.. kivipii?

3: Kocha wa Simba alikuja na system ya 4-2-3-1 .. But kosa kubwa ni kubakia kwenye 'Style of Play' ile ile ya msimu uliopita.. Simba imepoteza utawala wake wa kumiliki mpira kwenye 'zone' ya mpinzani.

4: System ya 4-2-3-1 ilibebwa na ubongo wa CHAMA.. Bwalya ni mzuri lakini sio kila anayejua kupiga pasi anaweza kuwa mzuri kama namba 10! Inahitaji BRAIN ya kuichezesha Timu. Hatua nyingi za Bwalya zilikuwa karibu na Kanoute na sio Mugalu. Hii ikawapa kazi nyepesi Aucho na Bangala kupanga mambo yao

5: FEISAL SALUM 🙌 WHAT A PERFOMANCE🏅 Kucheza mbele ya Bangala na Aucho, Timu ikiwa na umiliki wa mpira ni kama kumkatia kiwanja cha pepo Feisal Salum.. Utulivu mkubwa, Pasi nyingi sahihi na uwezo mkubwa wa kukokota mpira ni silaha nzito iliyomtesa sana Lwanga

6: Ubingwa Safi lakini Nabi anatakiwa kuwa na sherehe fupi sana katika uwanja wa mazoezi. Perfomance ya Yanga kipindi pili ilionyesha bado timu haiko kwenye levo nzuri ya utimamu wa mwili. Bado Pacha ya Mwamnyeto na Dickson ina makosa mengi ya kuboresha

7: KANOUTE anajua mpira! Pasi nzuri sahihi kutoka mguuni mwake.. Lakini huwezi kushinda kirahisi mechi ya mpira wa miguu kwa kutegemea 'individual quality' pekee. Syteam ya Simba kipindi cha pili 4-1-3-2 angalau imempa Gomes somo la kufanyia kazi katika uwanja wa mazoezi

8: AUCHO.. THE TRANSFOMER🙌 Hana mambo mengi, Pasi pasi pasi ndio somo alilofaulu zaidi kwenye maisha yake ya soka!

9: BANGALAAA! Yule mwanaume ni ishara ya ubora wa uwekezaji uliofanywa na Yanga katika dirisha la usajili msimu huu! Anakaba, anashambulia! What A Player

10: Mugalu alishinda vita dhidi ya mabeki wa kati akashindwa kushinda vita ya kuweka mpira kambani. Nilipenda jinsi Tshabalala na Djuma walivyochagua kuheshimiana

Nb: Waliuza CHAMA wakanunua MABASI 😀
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad