WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye kombe la Shirikisho Barani Afrika, Biashara United ya mkoani Mara, jana Septemba 10, imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1 -0 dhidi ya Fc Dikhil ya Djibout .
Goli pekee la Biashara liliwekwa kimiani na Denis Nkane dakika 62 ya mchezo na kuweka hai matumaini ya kusonga mbele kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa Septemba 18.
Licha ya changamoto za kupata visa ambazo ziliwafanya kuchelewa kuanza safari waliwasili Djibout jana asubuhi na mechi kuchezwa jioni, wamefanikiwa kupambana na kuondoka na ushindi ugenini.