NCHI ya Afghanistan imeendelea kutikisa vichwa vya habari duniani baada ya kundi la Taliban kuipindua serika iliyokuwa madarakani na Rais wa nchi hiyo, Ashraf Ghani, kukimbia nchi yake. .
Katika hali ya kushangaza, kundi la Taliban limeweza kuteka miji mingi nchini humo isiokuwa bonde la Panjshir, kwa miongo kadhaa iliyopita bonde hilo limekuwa ngome imara hata mwaka 1980, Jeshi la Sovieti lilishindwa kuukabili ulinzi mkali wa bonde hilo.
Mwaka 1990 Taliban pia ilifanya majaribio ya kuvamia bonde hilo na matokeo yake kundi hilo lilipigwa vibaya.
Kundi lililoweka ngome kwa sasa kwenye bonde hilo ni National Resistance of Afghanistan (NRF) akizungumza na BBC kiongozi wa NRF Ali Nazary anasema ”Jeshi la Serikali na washirika wake walishindwa na Taliban pia walijaribu takribani miaka 25 iliyopita lakini walikutana na kipigo kibaya”
Bonde hilo lina kina kirefu na limejaa vumbi na udongo liko maili 75 sawa na kilometa 120km kusini magharibi kwenda kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.
Bonde hilo pia limetawaliwa na milima mirefu yenye urefu wa futi 9,800 kama kilometa tatu kutoka usawa wa bonde lenyewe.
Panjshir sio bonde moja kuna vibonde vidogo 21, pia linafahamika kwa uchimbaji wa madini pia milima inayo lizunguka bonde hilo ni ulinzi kwa watu wanaoishi humo ili wasifikiwe kirahisi.