Bondia aliyemtwanga Anthony Joshua apokewa kishujaa




Bondia, Oleksandr Usyk amepokewa kishujaa nyumbani kwao Ukraine baada  ya kufanikiwa kumtwanga Anthony Joshua katika pambano lililofanyika usiku wa Jumamosi jijini London.



Usyk bingwa wa uzito wa juu alifanikiwa kutwaa mikanda ya WBA (Super), IBF, WBO na IBO baada ya kumpiga Muingereza, Joshua kwa ushindi wa pointi za majaji wote (Unanimous Decision) katika uwanja wa Tottenham Hotspur Stadium na kuendelea na rekodi yake ya kutopigwa kwenye jumla ya mapambano yake 19 ambapo kati ya hayo 13 akishinda kwa KO.



Bingwa huyo ametua kwenye uwanja wa ndege wa Kiev’s Boryspil International na kupokewa na mashabiki, wanamasumbwi na waandishi wa habari huku uso wake ukionena kuwa na alama katokana pambano hilo.



Usky aliyehama uzito mwaka 2019 kutoka Cruiserweight kwenda Heavyweight, ameshinda kwa (117-112) (116-112), (115-113) baada ya kumalizika raundi zote 12.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad