Habari zilizotufikia hivi punde ni kuwa Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Mhe.William Ole Nasha amefariki dunia nyumbani kwake Jijini Dodoma.Taarifa zaidi tutawajuza wasomaji wetu kuhusu chanzo Cha kifo Cha Mhe Ole Nasha.
Taarifa hiyo imethibitishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
“Nasikitika kuwajulisha kuwa aliyekuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji Mhe. William Tate Ole Nasha amefariki dunia Jijini Dodoma. Natoa pole kwa Spika Mhe. Job Ndugai, Wabunge, Familia na Wananchi wa Ngorongoro. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina.”- Rais Samia.