Ujerumani imemchagua mbunge wa kwanza mwanamke mweusi




Awet Tesfaiesus ambaye ni mbunge wa chama cha Green atakuwa mwanamke wa kwanza mwenye asili ya Afrika ,kuchaguliwa kuwa mbunge katika bunge la Ujerumani-Bundestag.

Wakili huyo mwenye miaka 47-aligombea Hessen ambalo linahusisha Frankfurt na Kassel ambako anaishi.

Tangu amehitimu chuo kikuu cha Frankfurt mwaka 2006, amekuwa mwanasheria, mara nyingi akiwakilisha kesi za wakimbizi na wanaotafuta makazi, vyombo vya habari vya ndani vimeripoti.

Alizaliwa Eritrea, na kuhamia Ujerumani na familia yake akiwa ma umri wa miaka 6 na amekuwa katika mji wa Heidelberg.

Amekuwa mwanachama wa Greens tangu mwaka 2009, alijikita kwenye siasa kufuatia mapigano ya risasi ya Hanua nje tu ya Frankfurt, mwaka 2020 ambapo wanaofuata mrengo wa kulia waliuawa watu 11.

Jina lake, “Awet”, ambalo kwa asili ya lugha yake ya Eritre ina maanisha ushindi- “jina linateta nuru ya kuongoza njia katia methali za Eritrea.

Ataenda Berlin kuwa mbunge wa Bundestage.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad