Bunge la mpito la Mali latoa msamaha kwa viongozi wa mapinduzi





Viongozi wa mapinduzi mawili ya hivi karibuni nchini Mali wamepewa msamaha nabunge la mpito la nchi hiyo.

Kanali Assimi Goïta na waaafisa wengine wa kijeshi waliohusika katika kumuondoa mamlakani Rais Ibrahim Boubacar Keïta mwezi Agosti mwaka jana na rais wa mpito, Bah Ndaw, mwezi Mei mwaka huu, hawatakabiliwa na mashitaka.

Hoja hiyo ilipitishwa kwa wingi wa kura za wabunge katika baraza la taifa la mpito la Mali.

Kanali Goïta amesema kuwa ataheshimu ukomo wa Februali 2022 , tarehe ambayo aliahidi uchaguzi wa serikali ya kiraia utafanyika.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad