Burna Boy Aamua Kujipa Likizo Kutoa Album Afunguka Haya



August 12,2013, @burnaboygram aliachia Album yake ya kwanza aliyoipa jina la L.I.F.E ikiwa ni kifupi cha LEAVING AN IMPACT FOR ETERNITY iliyouuza zaidi ya nakala elfu 40 kwa siku yake ya kwanza toka iachiwe.

Msanii huyo ambaye aliingia rasmi kwenye game ya muziki mwaka 2011, ana miaka 10 akiwa na album 5 mkononi na EP 2 huku albamu mbili za AFRICAN GIANT na TWICE AS TALL zikiwa ni albamu zilizompa mafanikio zaidi kwenye soko la muziki Duniani.

2020 albamu yake ya African Giant iliyotoka July 26,2019 iliingia kwenye nomination za tuzo kubwa duniani (Grammy) lakini tuzo hiyo ilichukuliwa na mwanamama mwenye jina refu balaa tokea nchini Benin, Angélique Kpasseloko Hinto Hounsinou Kandjo Manta Zogbin Kidjo ( @angeliquekidjo ). Na akiidedicate tuzo hiyo kwa Burna Boy huku akiwaambia Grammy kuwa Burna is coming.

2021 kupitia Albamu yake ya Twice as Tall iliyotoka August 14,2020,Burna Boy alifanikiwa kuondoka na tuzo ya Grammy kwenye kipengele kilekile cha Best Global Music Album ambacho awali kilifahamika kama Best World Music Album.

kupitia Insta story yake hii leo Sept 18, Burna amedai anaweza asiachie Albamu kwa muda mrefu hadi pale atapo toa taarifa rasmi. Dizaini kama ameamua kujipa breki japo stock ipo ya kutosha.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad