CCM yawasubiri Gwajima, Silaa





Baada ya Bunge kuwatia hatiani wabunge wawili wa CCM, Askofu Josephat Gwajima na mwenzake Jerry Silaa, kwa kukiuka maadili ya Bunge na kuagiza chama kichukue hatua dhidi yao, viongozi wa Chama cha Mapinduzi Ilala na Kinondoni wanasema wanasubiri maelekezo rasmi juu ya adhabu za wabunge hao.
Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Shua Mwasanguti alisema licha ya kusikia maelekezo ya Bunge, bado wanasubiri maelezo ya Askofu Gwajima. Naye Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Idd Mkowa alisema wanasubiri maelekezo kutoka makao makuu ya chama hicho kuhusu sakata la Silaa.

“Bunge wametoa mapendekezo yao yatakayowasilishwa makao makuu ya CCM kisha watashusha ngazi ya wilaya ambapo tutapewa maelekezo ya kufanya. Tukipewa maelekezo tutaitisha kikao cha kamati ya maadili kwa ajili ya kumsikiliza Silaa.

Mkowa alisema kwa sasa ni vigumu kuainisha adhabu atakayopewa Silaa, ingawa zipo nyingine, ikiwemo onyo au karipio, lakini itategemea maelezo katika kikao cha kamati ya maadili ya wilaya kitakachokuwa na wajumbe watano.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad