Watu Wanne wamejeruhiwa vibaya baada ya Chui kuvamia eneo la makazi ya watu Bomani kata ya Bomang'ombe katika wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.
Tukio hilo limetokea mapema asubuhi ya Septemba 29.2021 kabla ya kudhibitiwa na askari Polisi kwa hatua za awali.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema askari wamefanikiwa kudhibiti wananchi wasipate madhara zaidi kabla ya askari wa wanyama pori kufika katika eneo hilo.
"Chui alionekana eneo la jirani na Zafanana amejeruhi watu wanne na kisha baadae wananchi walipoanza jitihada za kumkabili aliingia katika nyumba ya kulala wageni na kisha kumjeruhi dada mmoja ambaye inadaiwa dada huyo alikuwa akifanya usafi."alisema mmoja wa mashuhuda hao.
Tayari majeruhi hao waliitambulika kwa majina ya Emmanuel Urassa(37)Jesca Nkoo(21) Urusula Cosmas (26) na Maliki Sakia (31) wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Hai.