CHUO kikuu cha Ryerson kilichopo Toronto, Canada kimeanzisha kozi ya mastaa wawili watokao nchini humo Aubrey Drake Graham maarufu kama Drake pamoja na Abel Makkonen Tesfaye maarufu kama The Weekend itakayoanza rasmi mwakani 2022.
Unaambiwa katika kozi hiyo wanafunzi wa hapo watajifunza kuhusu rekodi mbalimbali zilizowekwa na mastaa hao pamoja na safari yao ya muziki kwa ujumla , uongozi wa chuo hicho umethibitisha kuanza kozi hiyo mapema mwakani.
Kuna kozi nyingine nyingi zinafundishwa katika chuo hicho lakini hii ni wazi kabisa inaonekana kupendwa na Wanafunzi wengi wa chuoni hapo, Suala hili ni lakujiuliza kwa vyuo vingi vya Afrika je kuna hiki kitu ama hakuna , na kama hakuna nini kifanyike dhidi ya suala hili kwani mataifa yalioendelelea yanajitanua katika nyanja mbalimbali na suala la muziki kuonekana kama biashara ama ajira na sio uhuni kama ilivyokua mwanzo .
Lakini ifahamike tu kwamba haya maisha yanaitaji mfano wa kuigwa watoto wa mjini wanaiita ‘ role model ” kwa hivyo suala la wasanii hawa wawili kusomwa katika chuo kikuu ni chachu kwa vijana wa nchi hiyo , kwa hivyo basi sio mbaya pia hata hapa bongo ikianzishwa kuwasoma wasanii wakubwa ikiwa ni moja ya chachu ya maendeleo kwa vijana.
Swali la kizushi je kwa hapa bongo ni wasanii gani utapenda wasomwe katika vyuo vikuu????