Dereva wa Marehemu Ole Nasha Asimulia Hali ya Marehemu Kabla ya Umauti "Alikataa Kwenda Hospitalini"



Fikiri Madinda ambaye ni dereva wa aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Mhe. William Tate Ole Nasha, ameeleza kauli ya mwisho ya Naibu Waziri huyo kabla ya umauti kumkuta jana Septemba 28, 2021.

“Tumelala Arusha kuamka asubuhi wakati namchukua kuanza safari akasema leo usiku hali yangu ya presha haikuwa nzuri nadhani hali ya hewa sio nzuri akasema niko vizuri nadhani tunaweza kuendelea na safari mpaka tumefika Dodoma akasema kesho saa tatu nipitie twende ofisini tulivyomuacha hapo ndio ilikuwa kauli yake ya mwisho.


“Baada ya muda napigiwa simu Boss wako anaumwa kufika naambiwa na Majirani naambiwa alipata shida ya kuingia mlangoni tukamsaidia kuingia baada ya kuingia akasema anajisikia vibaya lakini aliweza kununua mpaka umeme akaweka akaomba maji.


“Wakasema wampeleke hospitali alikataa akasema subiri nipumzike kwanza nitapata nafuu halafu nitawaambia basi hakuweza tena kupata nafuu ndio umauti ukamkuta,” amesema Fikiri Madinda.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad