Emanuel Okwi Aibukia Simba Day, Shangwe Kama Lote Akisalimia Wananchi




MCHEZAJI wa zamani wa Klabu ya Simba Emmauel Anold Okwi ameibukia katika Simba Day na kuibua shangwe kwa mashabiki na wapenzi wa Simba waliojitokea maelfu kwa maelfu Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Slaam.

Okwi ambaye alijiunga na Simba mwaka 2009 akiwa na umri wa miaka 18 ameichezea klabu hiyo ya Wekundu wa Msimbazi kwa mafanikio makubwa hasa kutokana na uwezo wake wa kusakata kabumbu uwanjani. Aliondoka Simba 2019 lakini hadi leo amebaki kuwa kipenzi cha wana Simba.

Hivyo tangu alipoondoka hajawahi kuonekana katika Uwanja wa Mkapa na mbele ya Wana Simba hadi leo Septemba 19,2021 ambako ameibuka na kuanza kuzunguka uwanjani akisalimia mashabiki.

Okwi aliingia uwanjani saa 8:15 mchana ambapo alianza kusalimia wana Simba kuanzia upande wa kulia na kisha kuelekea upande wa kushoto wa Uwanja wa Mkapa na wakati anasalimia alivaa jezi ya Simba .Muda wote wakati anapita uwanjani alikuwa akisalimia kwa kunyosha mikono juu .

Wakati wote huo mashabiki wa Simba waliamua kumuonesha heshima ya upendo kwa kusimama muda wote huku wakimshangilia.

Mbali ya Okwi kusalimia mashabiki wa Simba,aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba Mzee Hassan Dalali alipata nafasi ya kupita uwanjani akisalimia mashabiki.Mzee Dalila alizunguka uwanja mzima huku akionesha kutopita na wakati kwani kuna nyakati alikuwa akisakata Singeli kiasi cha kufanya Wana Simba kumshalingilia.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad