Fahamu Historia ya Hans Pope Ambae ni Baba Wa Zakaria Hans Pope Aliyeuawa Kinyama na Idd Amin



Mzee Hans Pope (Baba wa Zakaria) huyu mzee alikuwa RPC wa Kagera ambapo alikuwa akifanyia kazi wanajeshi wa Idd Amin walivamia sehemu ya TZ mwaka 1971 sio kwa nia ya vita bali kwa nia ya kuwaokoa wenzao ambao walijikuta wamezurula hadi sehemu ya TZ hivo wakaishia kutekwa na askari wa TZ

Kuna story nyingi juu ya sababu ya wanajeshi hao wa Uganda kuingia TZ lakini ya kuaminika ni kwamba walifika eneo la TZ kufuata maji na hivo wakatekwa wenzao walipopata taarifa waliona hawawezi ku report makao makuu ya jeshi la Uganda hili suala bali wakaamua kuja kuwaokoa wenzao


Wanajeshi wa Uganda ambao walikuwa ni wachache walifanya ujinga wa kuja na vifaru viwili na badala ya kuokoa wenzao walimkuta Hans pope (RPC) akiwa na dereva wake kwenye land Rover wakaamua kumfuata RPC alivoona anafuatwa na wanajeshi wa Uganda akaanza kukimbia akapige radio call kutaarifu makao makuu uvamizi wa wanajeshi wa Uganda, lakini kabla hajafikia Radio Call alipigwa risasi kwenye paja na akaanguka chini, dereva wake naye alivoona hivo alishuka na kuanza kukimbilia Radio call lakini naye alipigwa risasi ya mguu na kuanguka,akiwa chini huyo dereva alijaribu kushika bunduki ndipo akapigwa risasi nyingine mkononi na wanajeshi wa Uganda ambao walifika na kumchukua RPC pope


Kwa mujibu wa mashuhuda RPC aliwasihi wanajeshi wa Uganda wasimuue lakini wakambeba na kwenda naye Uganda ambapo Idd Amin alitangaza kwamba Hans Pope ni mamluki wa kichina aliyevamia Uganda (hapa Idd Amin alidanganywa na wasaidizi wake), basi Hans pope aliteswa na kuuawa na baadaye aliwekwa mwili wake maonesho kwa siku tatu (uliwekwa dawa usiharibike)

Baada ya hapo wanajeshi wa Amin waliupeleka mwili wa Hans pope huko hospitali ya Mulago na kuwapa madaktari kisha wakaondoka bila kutoa maelekezo,Madaktari waliamua kwa siri kubwa kuchukua jukumu la hatari la kuuwekea kemikali za kuutunza kwa miaka 30. Lakini ilikuwa kazi ngumu kwa sababu marehemu Hans pope alidungwa visu karibu kila sehemu ya mwili na alikuwa na majeraha ya risasi hivo basi dawa za kutunza mwili alizochomwa zilitokea kwenye mashimo ya vidonda


Baada ya miaka 8 Idd Amin alitolewa madarakani na mwili huo ulikabidhiwa kwa Serikali ya TZ ambapo ulizikwa huko Iringa.

Source:SwahiliForums

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad