"Gwajiboy Oyee, tunachanja au hatuchanji? haya Mh Mbunge (Gwajima) endelea"- Rais Samia wakati akimkaribisha Mbunge Gwajima kuongea
"Mh Rais ulituahidi kutupa bilioni 5 kwa ajili ya mafuriko ya hapo Chasimba ambayo kila mwaka watu wanakwenda na maji, nakuomba sana Mama kwa sababu umeshafika utatukumbuka kwa hayo"- Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima Jambo la mwisho Mama nakushukuru kwa kusimama kwenye jimbo la Kawe, sisi wana Kawe sio tu tunakupenda, tuna mahaba na wewe na tunakupenda sana sana"- Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima
"Nataka niwaambie kwamba tozo zitaendelea kuwepo, sababu tozo zile miezi miwili tuliyoanza nayo tumekusanya zaidi ya bilioni 60 na zimepelekwa kujenga vituo vya afya, tunajenga wenyewe ili wafadhili wanaokuja na masharti wasituingilie mambo yetu"- Rais Samia
"Wanadamu ukifanya watasema, usipofanya watasema, bora tufanye waseme lakini wakione, lakini wanasema kelele za mlango hazimuachishi mwenye nyumba kulala, lakini tuangalie tunakusanya fedha kwa ajili gani, maendeleo yakionekana msichoke"- Rais Samia
"Kazi ninayokwenda kuifanya ni kuitangaza nchi, nina crew ya wapiga picha wa kimataifa, wanachukua picha na kutengeneza filamu ya Tanzania na tunakwenda kuizindua Marekani na itaoneshwa ulimwengu mzima na itatusaidia kuleta wawekezaji na watalii"- Rais Samia