Msemaji wa klabu ya Yanga SC, Haji Manara amesema kuwa Yanga SC inakuwa timu ya kwanza toka Uhuru wa nchi kukodi ndege ya Shirika la ATCL, kwenda nje ya nchi kucheza mechi.
Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram, Manara ameandika kuwa Yanga ni timu ya wananchi lazima wasapoti mali za Watanzania na kuiunga mkono Serikali na Shirika la Ndege.
"Maana halisi ya Team
ya Wananchi ndio hii haijawahi kutokea toka Uhuru Club yoyote kukodisha ndege ya Shirika la kwetu wenyewe ATCL (Air Bus A 220-300) , kwenda nje kucheza mechi"
"Halafu hatukodishi kutupeleka Comoro au Nampula ni Nigeria Mjomba. Sio tu tunaikodisha bali itatusubiri hadi Jumapili usiku kuturejesha nchini baada ya mechi"
"Wananchi lazima wasapoti mali za Watanzania na kuiunga mkono Serekali yetu na Shirika kwa ujumla. Hii ndio Yanga na tutakachokwenda kukifanya Afrika itasimama Insha'Allah"
Yanga inatarajiwa kuondoka nchini siku ya Ijumaa kwenda Nigeria kucheza mechi yao ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United Septemba 19, 2021 katika uwanja wa Akokiye Amiesimake, Port Harcourt nchini Nigeria