Star wa Bongo Fleva na bosi wa Konde Music Worldwide, Harmonize amemtembelea Mama Janeth Magufuli mke wa aliyekuwa Rais wa Tanzania wa awamu ya 5 John Pombe Magufuli nyumbani kwake Chato.
Harmonize ame-share picha kwenye ukurasa wake wa instagram akiwa na Mama Janeth kwa mara ya kwanza tangu kifo cha Rais kilipotokea mwezi Machi 17, 2021 na kuandika ‘’(4) ever love (JPM) endelea kupumzika swahiba”.