Kaimu Afisa habari wa Klabu ya Simba, Ezekiel Kamwaga, amesema kuwa kuanzia leo, Septemba 3, 2021 jezi za simba zinapatikana katika maduka yote ya vunja bei.
“Maombi ya jezi kutoka kwa mashabiki wa Simba yamekuwa makubwa sana na uongozi umeona ni vyema kuwasikiliza. Natangaza rasmi kwamba kuanzia sasa jezi mpya za Simba zinapatikana sasa kwenye maduka ya Vunja Bei nchi nzima."- Ezekiel Kamwaga.