Na @johnharamba
Wakati Didier Gomes anatua #Simba aliikuta imefanikiwa kupiga hatua kubwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika chini ya Sven ambaye aliondoka muda mfupi tu baada ya mafanikio aliyoyapata.
Licha ya kuwa #Sven alikuwa na nafasi ya kuendeleza ushujaa wake, aliamua kuondoka kwa sababu zake binafsi, hivyo kuingia kwa Gomes aliikuta timu ikiwa katika MWENDO.
Ikawa rahisi kwake kuendeleza kile alichokikuta, hakubadilisha mambo mengi kwa kuwa kama ni wachezaji alikuta wapo fiti kuanzia kiakili hadi kimwili na chemistry ya wachezaji ilikuwa vizuri.
Simba ya sasa chini ya Gomes sasa ndiyo kama kazi imeanza, amepoteza wachezaji wawili waliokuwa key players, kuna maingizo mapya na pia wachezaji wametoka kwenye mapumziko.
Yote hayo yanafanya ni kama anaanza upya, huu ni muda wake wa kuonyesha kweli ana ubora unaotakiwa wa kuitoa timu katika daraja moja kwenda lingine au la, na huu ni moja ya MTIHANI MGUMU SANA SANA kwa makocha wengi.
Ndiyo maana timu ikishapoteza muunganiko uwanjani inakuwa ngumu kwa kuwa kocha ni kama anakuwa anaanza kuifundisha timu mpya ambayo haijui.
Kibaya zaidi ni kuanza mwendo vibaya kwa kufungwa na Yanga.
Kwa uwekezaji wa Simba ulivyo, bila kujali hizo sababu nilizozitaja juu, kuna uwezekano mkubwa SAFARI YA GOMES ITAKUWA INANUKIA.
Mtihani mgumu ni kuitengeneza SIMBA YAKE siyo samba aliyoikuta.
Wakati akipambana na hilo, akumbuke kuwa kuna Ligi ya Mabingwa inamsubiri, kuna Yanga ambao baada ya kutolewa kimataifa nguvu zao zote zitabaki Ligi Kuu Bara, hapo ndipo tutakapouona USHUJAA WA GOMES.
Kitendo cha VIONGOZI WA SIMBA KUONEKANA KAMA WAMESUSIA MEDALI uwanjani ni wazi kuwa hawajayachukulia poa matokeo ya kufungwa 1-0 na Yanga, GOMES AJIANDAE!