House Girl ‘Alivyoimaliza’ Familia Hii Kizembe






SIKIA kisa hiki cha mke ambaye alimhisi mumewe kuwa anatembea na mfanyakazi wao wa ndani (housegirl) kutokana na ukweli kuwa, housegirl yule alikuwa mzuri mno kimuonekano, kiumbo na kwa sura.

 

Alifikiri kumfukuza lakini mumewe aligoma kabisa kutokana na uchapakazi wa binti yule. Hivyo, hakuona sababu ya msingi ya kumfukuza mtoto wa watu bila sababu ya msingi.

 

Hakika housegirl alikua akizidi kumnyima usingizi mke wa bosi wake. Kadri siku zilivyozidi kwenda, housegirl alizidi kumeremeta huku akiikereketa roho ya mama. Kila nguo aliyovaa ilimpendeza. Kila mkao aliokaa alionekana ni wa kimitego na hofu iliendelea kutanda kwa mke wa boss.

 

Mke alizidi kuhisi mabaya na mbaya zaidi kila siku usiku wakati mmewe akiaga kuwa anaenda kuangalia mpira sebuleni baada ya muda mfupi mke alikuwa anasikia miguno chumba mwa housegirl hivyo akajua itakua tu ni mumewe huwa ananyata na kumuingilia housegirl wao ndio maana mume shughuli chumbani siku za karibuni ilionekana kumshinda kwa kuchoka haraka mno.

 

Basi weekend moja mama yule akaamua kumtuma housegirl kijijini kwa safari ya siku mbili kwenda kijijini kwao na mama yule kupeleka mahitaji kwa wazee wake, bila kumjulisha mumewe wala mtu yeyote pale nyumbani.

 

Usiku ule wa Jumamosi mume alimwambia mkewe utaratibu wake wa kawaida kuwa anaenda kuangalia mpira kwenye tv ya sebuleni kwao.

 

Kama kawaida, mke alikubali na mume akaenda sebuleni. Mke taratibu akanyata na kuzama chumbani kwa housegirl, akasaula nguo zote akabaki uchi wa mnyama kama alivyozaliwa, akajilaza kitandani.

 

Baada ya muda kidogo, alisikia mlango ukifunguliwa taratibu akaingia mtu akapanda kitandani na bila kuuliza akavua nguo akaanza kula tunda.

 

Shughuli imekolea sasa, tena vurugu mechi, jamaa ile anafunga bao la tano, mke akapagawa, uzalendo ukamshinda akajikuta anaropoka…

 

“Inatosha, leo nimekukamata, kumbe hivi ndivyo huwa unafanya na housegirl wakati ukiwa na mimi bao moja tu unasema umechoka? Mchezo wako huu ndiyo unakumaliza nguvu na ukija chumbani kwangu unasema umechoka wakati hapa tayari mabao matano na unataka uendelee?”

 

Msala huu tayari, jamaa akapigwa butwaa kama amechomwa ganzi, kwa mshituko, ghafla jamaa akajibu, “Samahani mke wa boss sikujua kama ni wewe. Mimi ni houseboy wenu mkata majani; nisamehe tafadhali!”

 

Mke alishtuka sana, akapiga kelele kwa nguvu maana alimjua houseboy wao kuwa ni mwathirika wa UKIMWI. Walimuajiri ili kumsaidia kwa kuwa kijana yule ni yatima, alizaliwa na UKIMWI kwani wazazi wake wote wawili walipofariki alitengwa na ndugu ndipo wakamsaidia kwa kumuajiri ili akate majani, kuzibua vyoo.

 

Kelele alizopiga mama zilimkurupusha mmewe sebuleni na kuwasha taa za nyumba nzima kisha akaelekea chumba cha housegirl kujua nini kimemsibu mkewe. Alipoingia hakuamini macho yake kwa kumwona mkewe akiwa uchi wa mnyama kama walivyozaliwa tena kitandani akiwa na houseboy wao akimbembeleza.

 

Baba yule masikini alishindwa kuelewa nini kimetokea, akawa anahisi ni kama anaota ndotoni, mkewe amepigwa ganzi, houseboy hana la kufanya, housegirl yupo kijijini kwao na mke wa bosi, basi baba huyu alianguka ghafla akapoteza fahamu, wamempeleka hospitali tayari ameshakuwa marehemu.

 

Kumbukua mama huyu tayari ameukwaa UKIMWI wa houseboy, baada ya mazishi ya mumewe, siku chache baadaye mama yule akaaga dunia kwa kunywa sumu kwani alishindwa kuisitiri aibu yake mbele ya uso wa dunia na familia yake.

Nini umejifunza?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad