Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro amesema watakuwa wakipita katika Nyumba za Ibada kukagua mafunzo wanayofundishwa watoto katika Madrasa na Shule za Jumapili (Sunday Schools)
IGP Sirro ameongeza kuwa hatua hiyo ni kutaka kufahamu aina ya mafundisho yanayotolewa maeneo hayo, jambo ambalo amejifunza Rwanda alipokwenda kwa ziara ya siku nne
Amesema watawashirikisha Viongozi wa Dini na Timu ya Kupambana na Makosa ya Kigaidi kuona namna ya kupitia mafunzo hayo kuona kama yanawajenga au yanawabomoa