Jasusi Mwanamke Apotea, Rais na Waziri Mkuu Watofautiana





KUPOTEA kwa Ikran Tahlil ambaye ni wakala wa Shirika la Kitaifa la Ujasusi na Usalama (Nisa) nchini Somalia mnamo Juni limesababisha mgawnayiko ndani ya serikali baada ya rais na waziri mkuu wa nchi hiyo kutoa amri zinazokinzana.



Ikran Tahlil alivyotokweka.

Nisa ilisema wiki iliyopita kwamba Ikran Tahlil, ambaye alifanya kazi katika idara ya usalama ya mtandao wa shirika hilo, aliuawa na kundi la wanamgambo wa al-Shabab baada ya kumteka nyara kutoka mji mkuu Mogadishu. Kundi la wapiganaji wa Al-Shabab lilikana kuhusika katika kutoweka kwa Tahlil na madai ya kumuua.

 

Waziri Mkuu Mohamed Roble alitoa taarifa ya video mnamo Septemba 4, mwaka huu na kusema kwamba maelezo ya shirika hilo la ujasusi juu ya mwanamke huyo aliyepotea hayakuwa “ya kuridhisha”.


Mama mzazi wa Ikran Tahlil.

Siku moja baadaye, alitangaza kufutwa kazi kwa Mkurugenzi wa Nisa, Fahad Yasin, na kumteua Luteni Jenerali Bashir Mohamed Jama’a kukaimu kwa muda.

 

Lakini Rais Mohamed Abdullahi Farmajo alitupilia mbali agizo la waziri mkuu, akimwamuru mkuu wa upelelezi kubaki ofisini, ili ripoti Televisheni ya serikali.



Kesi ya ajenti huyo wa Nisa imeibua taharuki za kisiasa nchini Somalia, huku wanasiasa wakilifanya suala la kampeni katika uchaguzi unaoendelea na habari za kutoweka kwake kusambaa sana kwenye mitandao ya kijamii.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad