Gomes Aja na Pacha Mpya ya Mabao Simba




HATIMAYE Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes, amekamilisha kazi iliyompeleka kwenye maandalizi ya msimu ujao wa michuano mbalimbali kwa kuunda pacha mpya ya mabao.


Sasa ni rasmi kikosi chake cha kwanza katika safu ya ushambuliaji, kitaongozwa na Chris Mshimba Mugalu ambaye atapewa sapoti na Rally Bwalya na Sadio Kanouté raia wa Mali.

 

Msimu uliopita, pacha ya Gomes, ilikuwa ikiundwa zaidi na Clatous Chama raia wa Zambia, Luís Miquissone raia wa Msumbiji na John Bocco jambo ambalo sasa limebadilika baada ya wawili kati yao kuondoka, hivyo imemlazimu kuunda jeshi jipya la viungo washambuliaji ambao ni Bwalya na Sadio.

 

Chanzo chetu kutoka ndani ya Simba kimeliambia Championi Jumatano kwamba, tayari Gomes ameshakamilisha kazi yake ya kuunda pacha mpya, ambapo amefanikiwa kuwaunganisha vizuri Bwalya, Sadio Kanouté na Mugalu.

 

“Kwa namna ambavyo Gomes ametengeneza pacha mpya ndani ya kikosi chetu, hakika sina shaka na upatikanaji wa mabao, kwani tangu aanze kuwaandaa Bwalya na Sadio kama wapishi wa Mugalu, mambo yanajionyesha wazi kabisa kuwa mvua ya mabao itaendelea kuzinyeshea timu pinzani msimu ujao,” kilisema chanzo hicho.

 

Championi lilimtafuta Kaimu Ofisa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ezekiel Kamwaga ili atuhakikishie hilo, ambapo alisema: “Kazi ya kocha baada ya Miquissone na Chama kuondoka, ilikuwa ni kuhakikisha anaunda jeshi jipya, hivyo hadi muda huu ni nkweli ameshaunda vijana wanye uwezo mkubwa.

 

“Ninachoweza kukwambia tu ni kwamba, Bwalya wa sasa kakua, hivyo anafanya mambo ya kiutu uzima, baada ya kutoonekana sana msimu uliyopita mbele ya Chama na Miquissone, sasa ni kweli ameamka na mambo yote haya nawaomba wapenda mpira tukutane Jumapili ndani ya Dimba la Mkapa ili wapate burudani ya mabao.”

MUSA MATEJA, Dar es Salaam

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad