Johnson & Johnson wasitisha majaribio ya Chanjo ya Ukimwi Afrika




Mnamo 2019, watu milioni 38 walikuwa wakiishi na VVU duniani.
Mnamo 2019, watu milioni 38 walikuwa wakiishi na VVU duniani. iStock / jarun011
Huu ni mpango wa majaribio, unaoitwa Imbokodo, ambao ulianza mnamo mwaka 2017 katika nchi tano kusini mwa Afrika. Kwa kukosekana kwa matokeo kamili, "mpango wa majaribio ya Imbokodo hautaendelea," kampuni hiyo ya dawa kutoka Marekani ilitangaza Jumanne (Agosti 31) katika taarifa kwa waandishi wa habari.

Ni jambo la kusikitisha na kutamausha katika vita dhidi ya ugonjwa huu ambao unaathiri watu milioni 38 ulimwenguni, wengi wao wakiwa katika bara la Afrika, na ambao utaftaji wa chanjo haujafanikiwa kwa miongo kadhaa. Kampuni ya Johnson & Johnson imeamua kusitisha mpango wake wa Imbokodo.

Mpango huu wa majaribio ni ushirikiano kati ya kampuni ya dawa kutoka Marekani, Bill & Melinda Gates Foundation, na serikali ya Afrika Kusini.

Wanawake wasiopungua 2,600 wenye umri wa miaka 18 hadi 35 kutoka Malawi, Msumbiji, Zambia, Afrika Kusini na Zimbabwe walishiriki katika jaribio hili la kliniki. Nusu yao walipokea sindano nyingi za chanjo hii ya majaribio.

Lakini miaka miwili baada ya sindano ya kwanza, matokeo yalionekana hayafai. "Hata kama chanjo hiyo ilitumiwa vizuri, ufanisi wake ni 25% tu," kampuni ya J & J imebaini.

Kampuni hii pia imethibitisha kuwa inaendelea na mpango mwinine wa majaribio, uitwayo Mosaico, ambao unachunguza chanjo, na muundo tofauti, kwa wanaume huko Amerika na Ulaya. Na majaribio hayo ymepangwa kumalizika mwezi Machi 2024

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad