MKUU wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo ameunga mkono kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoitoa leo ya kwamba mwaka 2025 atagombea Urais hivyo ni wakati wa wanawake kuingia Ikulu kwa kupigiwa kura.
“Ni kweli kabisa 2025 ni mwaka wa kumuweka Rais Mwanamke Ikulu, ni wakati sasa wa wanawake wote kuungana na kutumia fursa hii kufanikisha hili na kuendelea kuandika historia Tanzania, naamini wanaume pia watatuunga mkono maana nia ya Mama kulitumikia Taifa letu wote tumeiona.
“Lakini pia kwa kutambua Wanawake tumefanya kazi kubwa kuleta uhuru wa nchi yetu, kujenga siasa za nchi yetu na pia Kama Mhe. Rais alivyosema tumekuwa chachu nyuma ya Wanaume wengi kupata vyeo vya juu, ni wakati wetu sasa!!! Namuunga mkono Mama, 2025 twende na Mama.” – amesema Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo.