Kagera Sugar Yaikamua Simba Milioni 40, Kisa Mhilu





RASMI sasa Yusuph Mhilu ni mali ya Simba baada ya uhamisho wake kukamilika na mabosi wa Simba kuweka mkwanja mezani kwa ajili ya kuvunja mkataba wake.

 

Taarifa rasmi kutoka Kagera Sugar imeeleza namna hii:”Tumefikia makubaliano ya pande zote mbili (Kagera Sugar FC na Simba SC) juu ya uhamisho wa aliyekuwa mchezaji wetu Nyota Yusuph Valentine Mhilu kwa Dau la Tsh.40M.

 

“Yusuph Mhilu alisaini kandarasi ya miaka miwili kuitumikia Kagera Sugar Football Club mwaka jana 2020. Hivyo uhamisho huu wa Yusuph Mhilu kwenda Simba ni Uhamisho ambao umehusisha kuvunja mkataba wake wa mwaka mmoja uliosalia ndani ya Klabu ya Kagera Sugar.

 

“Tunamtakia kila la kheri huko aendako na Mungu amsimamie katika kukiendeleza kipaji chake,”.

Usajili wa Mhilu kuibukia Simba ulikuwa ni wa ghafla baada ya viongozi wa Simba kumdaka mazimamazima Dar alipotoka na timu ya taifa ya Tanzania kwa vijana chini ya umri wa miaka 23 kushiriki Cecafa.

 

Alisaini dili la miaka mitatu jambo ambalo liliwafanya mabosi wa Kagera Sugar kushangazwa na suala hilo la utambulisho kwa kuwa hakukuwa na taarifa kwao.

Kwa taarifa hiyo ni wazi kwamba Mhilu msimu ujao atakuwa ndani ya Simba kuendelea kupambania namba.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad