Asif Hasan Kerim, mmoja wa makamanda muhimu wa Hashd al-Shaabi, alifariki kutokana na mlipuko wa bomu lililotegwa kwenye gari lake huko Babeli, Iraq.
Kulingana na vyanzo kutoka Idara ya Polisi ya Babeli, Asif Hasan Kerim, Kamanda wa Operesheni ya Hashd al-Jazeera, alifariki katika eneo la mlipuko wa bomu lililotegwa kwenye gari lake katika mkoa wa Jeref an-Nasr.
Watu wawili walioandamana na Kerim pia walijeruhiwa.
Chanzo kimoja ambacho hakikutaka kutajwa jina, kiliripoti kwamba mkoa wa al-Uweysat, ambapo tukio hilo lilitokea, ulikuwa chini ya udhibiti wa Hashd al-Shaabi.
Hakuna mtu aliyedai kuhusika na mlipuko huo.