Kamwaga "Ninaondoka Simba Hivi Karibuni"




Ezekiel Kamwaga ambaye ni Kaimu Afisa habari wa Klabu ya Simba SC amesema klabu hiyo inaendelea na mchakato wa kumtafuta afisa habari kwani yeye ataondoka hivi karibuni kwenda nchini Uingereza.
“Ninakaimu nafasi ya Afisa Habari kwa muda wa miezi miwili, mwezi ujao nitakuwa naondoka Simba naenda UK, hivyo klabu itamtangaza Afisa Habari mpya. Mchakato unaelekea kukamilika.
“Simba ni ile ile, mashabiki ni wale wale niliowaacha 2013, kilichobadilika sana Simba, imeanza kuwa klabu yenye watu wenye heshima zao, sasa hivi kuna watu kama akina Dr Janabi, akina Mo Dewji, Barbara. Lakini pia sasa kuna mabadiliko kwenye social media.
“Simba Day ya mwaka huu itakuwa kubwa. Mpaka sasa tumeshapokea maombi ya timu ambazo zimeshashinda ubingwa wa Afrika zaidi ya mara mbili. Nawahakikishia Simba itacheza na timu kubwa sana barani Afrika katika Simba Day 2021.” – Ezekiel Kamwaga, Kaimu Afisa habari wa Simba SC.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad