Kauli ya Hassan Mwakinyo baada ya ushindi kwa TKO



 
Bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo amefanikiwa kutetea mkanda wake wake wa ubingwa wa African Boxing Union ‘ABU’ Middle Super Welter yaani wa uzito wa baada ya kumpiga bondia Julius Indongo kutoka Namibia kwa technical Knockout ‘TKO’ kwenye pambalo lililochezwa usiku wa kuamkia leo kwenye uk

Hassan Mwakinyo (Pichani) ambaye kwasasa amekuwa akifanya vizuri katika mapigano yake aliyopanda ulingoni.
Mwakinyo aliweza kumsukumia makonde mfululozo Julius Inbongo ambaye alipoteza mwelekeo na ndipo mwamuzi wa pamabano hilo akaamua kumaliza pambano zikiwa zimesalia sekunde 9 kukamilisha mzunguko wanne ilhali pambano hilo lilipangwa kuchezwa kwa mizunguko 12.

Baada ya ushindi huo Mwakinyo amesema; “Ushindi ni usajili wangu lakini sio nguvu yangu naamini ni nguvu ya watanzania wengi na pia nimefarijikia sana kumuona kiongozi wangu mkuu wa mkoa wa Tanga amefika hapa na baadhi ya viongoiz mbalimbali kutoka balozi za Tanzania, imenipa heshima sana”.

“Lakini niliwaambia mashabiki kuna tofauti ya bondia na professional boxing nikawaambia leo nitawaonesha nini maana ya professional boxing. Bondia niliyempiga hakuwa bondia mrahisika kama watu walivyokuwa wanafikiria, mumeona pambano la Tony lilivyopotea maana yake tumecheza na mabondia wakweli, Nashukuru kwa kufaulu mtihani huu”

Kwa upande mwingine bondia Julius Indongo amesema ameshangazwa na haelewi ilikuwaje mpaka Mwakinyo akaibuka na ushindi kwasababu ngumi nyingi mfululizo alizopigwa alikuwa anazikwepa.

“Kiukweli siwezi kusema chochote kuhusu mchezo huu, kwasababu nataka nirudie kujitazama na kuona kama nilipigwa na ngumi, labda kwasababu ukipigwa unaweza usijue umepigwa nataka kurudia na kuona nilipigwa na kushindwa kuendelea kwasababu niliona ngumi zake zinanikosa lakini akashinda, kiukweli sielewi kabisa nadhani ulikuwa mchezo wa upande mmoja”. Alisema Indongo.

Ushindi unamfanya Mwakinyo kuwa asilimia mia moja ya ushindi ya kimataifa kwenye ardhi ya nyumbani na kufikisha jumla ya mapambano 22 tokea aanze masumbwi miaka sita iliyopita na kushinda michezo 20 tena 14 akishinda kwa KOs na kupigwa michezo miwili pekee huku akiendelea kuwa bondia nambari moja kwa ubora Afrika, Tanzania na wa 24 Duniani kwa mabondia wa uzito wa kati pekee.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad