Kauli ya Ndugulile Baada ya Kutenguliwa Uwaziri na Rais Samia



Aliyekuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile, amemshukuru Rais Samia kwa kumpa nafasi ya kuhudumu ndani ya serikali yake kwa kipindi cha takribani miezi sita.


Dkt. Ndugulile ameandika maneno hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, mara baada ya kutenguliwa uteuzi wake juzi usiku na nafasi yake kuchukuliwa na Dkt. Ashatu Kijaji ambaye aliapishwa jana.


"Namshukuru sana Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kunipa fursa ya kuhudumu katika serikali yake, nawashukuru Wizara na Taasisi zake kwa ushirikiano walionipa, nashukuru wadau wa TEHAMA kwa ushirikiano mlionipa, hongera sana Dkt Ashatu Kijaji kwa kuteuliwa. Kazi Iendelee," ameandika Dkt. Ndugulile

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad