Kauli ya Polepole Baada ya Kuhojiwa na CCM




Kamati ya Maadili ya Wabunge wa CCM leo Ijumaa, Septemba 3, 2021 imewaita Dodoma kuwahoji Wabunge Jerry Silaa na Askofu Gwajima ambao Bunge lilipitisha azimio la kuwasimamisha mikutano miwili, ameonekana pia Mbunge Polepole akitoka kwenye mahojiano.



Askofu Gwajima na Silaa wameitwa na kamati kwa agizo la Bunge, wakidaiwa kusema uongo na kushusha hadhi ya Bunge, haikufahamika Polepole ameitwa kwa agizo la nani.

 

Baada ya kuhojiwa, Polepole aliongea kwa ufupi na waandishi wa habari akiwa ndani ya gari lake…. “Kikao cha maadili ni kikao cha ndani, kwa hiyo taarifa zote zitatoka kwa utaratibu wa chama, nawashukuru sana.”



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad