KESI ya uhujumu uchumi inayowakabili mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe yaanza Kusikilizwa





KESI ya uhujumu uchumi inayowakabili mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vya ugaidi leo Ijumaa, Septemba 3, 2021 imeanza kusikilizwa mahakama kuu divisheni ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi.



Leo kesi hiyo inaendelea katika hatua ya usikilizwaji wa pingamizi la awali lililowekwa na washtakiwa kupitia kwa jopo la mawakili wao 14 wakiongozwa na Peter Kibatala.


Katika pingamizi hilo washtakiwa hao wanadai kuwa hati ya mashtaka ina kasoro za kisheria pamoja na mambo mengine wakidai kuwa sheria ya ugaidi ambayo wanashtakiwa nayo haijafafanua viambato vya kosa la ugaidi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad