Kim Ashutumiwa Kuipigia Promo Sarafu ya Matapeli





SUPASTAA nchini Marekani, Kim Kardashian amekosolewa kwa kutangaza fedha ya kidigitali ambayo haijahalalishwa kwenye mtandao wake wa Instagram, na kiongozi wa mamlaka ya fedha nchini Uingereza.

 

Charles Randell amesema Kardashian aliwataka wafuasi wake mtandaoni ambao ni watu milioni 250, kubashiri tokeni ya kidigitali katika tangazo la Ethereum Max. Randell ameuita kuwa ni ubashiri wa tokeni ya digitali iliyotengenezwa mwezi mmoja kabla ya waanzilishi wake ambao hawajulikani.

 

Na aliwashutumu washawishi kwa kuchochea “udanganyifu wa utajiri wa haraka.” Randell alikuwa anazungumza hayo katika kongamano la kimataifa la uhalifu wa kiuchumi.

 

Mwenyekiti huyo alisema ujumbe wa Kardashian katika mtandao wa Instagram, ambao umewekwa kama tangazo, unaweza kupata uhamasishaji wa kifedha kwa wafuasi wengi wa mtu mmoja jambo ambalo ni historia.

 

Uhamasishaji wa tokeni inayofahamika kama Ethereum Max, alisisitiza kuwa usichanganywe na sarafu ya kidigitali ya Ethereum.

 

“Siwezi kusema kwa uhakika kuwa safari hii ni mbaya [Ethereum Max]. Lakini washawishi wa mtandaoni wamekuwa wakitumiwa na matapeli kuhamasisha sarafu mpya ambazo hazipo kabisa,” alisema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad