DADA mwenye ushawishi mkubwa wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, Kim Yo-jong anasema taifa hilo lipo tayari kuanza tena mazungumzo na Korea Kusini ikiwa itamaliza “sera zake za uhasama” Kim Yo-jong alikuwa akijibu wito mpya kutoka Korea Kusini kutangaza rasmi kumaliza vita vya Korea .
Wiki hii, rais wa Korea Kusini Moon Jae-in alitaka Korea mbili na washirika wao Marekani ambayo inaunga mkono Kusini, na China ambayo ni mshirika mkubwa wa uchumi wa Kaskazini – kutangaza kumaliza mzozo rasmi na kuleta amani katika peninsula hiyo ya Korea .
Lakini katika taarifa iliyotolewa Ijumaa kupitia vyombo vya habari vya serikali, Bi Kim alisema wazo hilo lilikuwa “la kupendeza”ameongeza kuwa Korea Kaskazini itakuwa tayari tu kujadili pendekezo hilo ikiwa Korea Kusini itaacha kile alichokiita “sera za uhasama” kwao.
“Kinachohitaji kutupiliwa mbali ni mitazamo ya kinafiki , ubaguzi, tabia mbaya na msimamo wa uhasama wa kuhalalisha matendo yao wenyewe huku wakikosoa utekelezaji wetu wa haki ya kujilinda,” alisema katika taarifa.
“Ni wakati tu sharti kama hilo litakapotimizwa, itawezekana kukaa uso kwa uso na kutangaza kukomesha mgogoro huo, ambao uligawanya peninsula hiyo kuwa nchi mbili, ulimalizika mnamo 1953.
Nchi hizo mbili zimekuwa kwenye vita tangu wakati huo, na zimekumbwa katika uhusiano wenye taharuki wakati mwingine .