Dada wa kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, Kim Yo Jong amesema Korea Kaskanzini ipo tayari kufikiria mkutano mwingine wa kilele na Korea Kusini endapo kutatolewa hakikisho la hali ya kuheshimiana kwa mataifa hayo mawili jirani.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na shirika la habari la Korea Kaskazini (KCNA) Wizara ya Muungano inatarajiwa kujiingiza haraka katika mazungumzo na serikali ya Pyongyang, huku ikitaka kuweka kiunganishi cha haraka baina ya mataifa hayo mawili.
Kauli ya Jong, inatolewa baada ya juma lililopita Korea Kaskazini kuzitaka Marekani na Korea Kusini kuachana na kile ilichokiita sera za kiuhasama na kuwa na undumi la kuwili katika jambo hilo, endapo kutakusudiwa mazungumzo kumalizia vita vya Korea vya 1950-53.