Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama Ray C ameamua kuanika majibu yake ya vipimo vya virusi vya Ukimwi alivyopima hivi karibuni.
Ray C ambaye aliwahi kutamba na vibao vikali kama vile ‘Mapenzi matamu’, ‘Na wewe milele’ na vinginevyo ameweka wazi kuwa hana maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Kupitia insta story yake, Ray C ame-share video fupi pamoja na picha inayoonesha cheti cha majibu ya kipimo cha ukimwi kilichoonesha kuwa hana maambukizi hayo, na kuwasihi watu kujipenda.