Kumekucha..Simba SC yathibitisha ujio wa TP Mazembe Simba day...Je Mnyama Atakufa Mbele ya Mashabiki zake?



Klabu ya Simba imethibitisha ujio wa kikosi cha mabaingwa mara tano wa Afrika, TP Mazembe kwa ajili ya kucheza mchezo wake wa kirafiki kwenye kilele cha Simba Day kinachotaraji kuadhimishwa siku ya Jumamosi ya Septemba 19 mwaka huu kwenye dimba la BW Mkapa.

Simba imethibitisha hilo kupitia ukarasa wake wa Instagram kwa kuandika  orodha ya wachezaji 23 wa TP Mazembe wanaotaraji kutua nchini siku za hivi karibuni kwa ajili ya mchezo huo wa kupamba na kutoa burudani kwa mashabiki, wanachama na wadau wa Simba SC.

Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Murtaza Mangungu mapema wiki hii alitolea ufafanuzi wa kwanini waliamua wababe hao wa DR Congo na si timu nyingine kwa kusema moja ya sababau ni Mazembe ni moja ya timu kubwa barani Afrika.

Mbali  na kigezo hicho Mangungu amesema, walitaka kucheza na miongoni mwa timu 10 bora Afrika kwa hoja kuwa zitatoa upinzani wakutosha kwa Simba kwani wapo makini ndani na nje ya uwanja licha ya kejeli za mashabiki wengine wakidau Mazembe imechuja.

Mangungu amemalizia sababu ya tatu kwa kusema, “Pia janga la corona limefanya mazingira ya timu kuingia na kutoka kwenye baadhi ya nchi kuwa magumu na kwenye baadhi ya nchi Ligi bado hazijamalizika,” hivyo Mazembe ikapatikana.

Mchezo huo pia ni kumbukizi ya mchezo wa robo fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika kwa msimu wa mwaka 2018-19 ambapo kwenye mcheza wa kwanza ulimalizika kwa sare ya bila kufungana kwa Mkapa na Simba kufunga 4 -1 Lubumbashi nchini DR Congo na hatimaye wawili hao walikutana tena Februari mwaka huu kwenye 'Simba Super Cup' ambapo pia walitoka sare ya bila kufungana.

Msafara huo utakuwa na wachezaji 23 na viongozi 12, na wachezaji hao ni;

Mounkoro Ibrahim,Saidi Baggio, Joseph Ochaya, Issa Mpeko Djos, Masengo Godest, Tandi Mwape, Ernest Muzolo, Mundeko Zetu, Koffi Koume, Zemanga Soze, Reinford Kalaba, Ettiene Mayombo, Sudi Bibonge, Bossu Bibonge, Beni Kizumbi, Baleke  Jean, Beya Joel, Ntambwe Kalonji, Marceil Ngimbi, Bileke Kelvin, Mika Michee, Arsene Zola na Bileke  Kelvin.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad