Kuna Kitu Yanga Wanapaswa Kujifunza Kwa Simba



Asubuhi nilisema kitu kuhusu GRB MODEL, nikasema ndio cycle sahihi kwa timu zetu huku Kusini mwa Jangwa, nikasema Simba ndio mfano mzuri wa hii kitu

Nikasema kwenye GRB MODEL kuna kitu kinaitwa GROWTH, nikimaanisha UKUAJI

Hapa kwenye Growth kuna vitu viwili vikubwa kwanza ni USAJILI! Ambapo nikasema Kuna saini ambazo wachezaji wanakuja kuikuza timu na baadhi wanakuja kukua na timu

Yanga wapo hapa! Na Simba waliwahi kuwepo hapa! Nilitaja saini za Yanga (rejea makala ya nyuma) ila kwa Simba walipokuwa hapa walileta watu wa kuikuza timu ambao wameproove sehemu kama Yanga walivyofanya msimu huu

Simba walileta watu kama Aishi Manula, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, John Bocco, Meddie Kagere, Chama na wengine ili waje kuikuza timu, ndipo hatua hii ya GROWTH, na ikamea vizuri sana

Ijapo wengi mlipiga kelele kuwa wanasajili wazee, lakini ndio ilikuwa inahitajika experienced players, ambao watakuja kuleta vitu viwili QR (Quick Reshuffle) na IS (Instant success) iwapo watafanikiwa

Kwenye hatua hii niambie Simba iliajiri Makocha wangapi? Unaweza kuona ndani ya miaka minne Simba wamesajili Makocha watatu tu na mmoja aliomba kuondoka!

Ikiwa na maana hatua hii ya GROWTH inatambulika kama ENTREPRENEUR PHASE! Unawekeza kwenye MUDA sambamba na RISK TAKING! Ni kitu ambacho Simba walifanya ila Yanga hawataki kufanya, wao wanatimua Makocha na kubadili vikosi

Ukitoka kwenye hii phase ndipo unakuja kwenye R! Ni RESULT ORIENTED! Ndani kuna ushindi na mataji! Hapa ndipo Yanga anapawaza bila kufata process

jr_farhanjr

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad