Kuna na Mapacha Wawili Walioungana, Wana Shirikiana Kutembea, Kuendesha Gari na Hata Kazi


UNAAMBIWA Mapacha wa Marekani Abigail Hensel (Abby) na Brittany Hensel wameungana hivi toka walipozaliwa March 07,1990 wakiwa na mwili mmoja lakini kila Mtu ana kichwa chake, moyo wake, tumbo lake , uti wa mgongo na hata mapafu yake pia.

Abby na Brittany kila mmoja ana mguu mmoja na mkono mmoja ambayo inafanya kazi kwa kushirikiana, kwahiyo hushirikiana kwenye kutembea, kupiga makofi, kuogelea, kukimbia, kuendesha Gari n.k ingawa wana uwezo wa kuongea, kula au kuandika kila Mtu kivyake.


Walizaliwa New Germany , Minnesota Marekani wakasoma hadi Elimu ya Chuo Kikuu, Bethel University na sasa wameajiriwa kama Walimu wakifundisha Sunnyside Elementary , New Brighton.

"Kwa sasa tunapata Mshahara mmoja kwakuwa tunafanya kazi ya Mtu mmoja kwa pamoja lakini katika siku zijazo tunafikiria kuongea na Maboss zetu watuongezee mshahara au kila Mtu apewe mshahara wake maana tuna Degree mbili kila Mtu yake na pia tunao uwezo wa kufundisha masomo tofauti kila mmoja au kufundisha kwa njia tofauti, mfano mmoja anaweza kuwa anafundisha huku mmoja anasimamia uelewa wa Wanafunzi na kujibu maswali Yao" ——— Abby

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad