Maafisa nchini Libya wamemuachilia huru mwanaye mmoja rais wa zamani wa Libya aliyeng’olewa mamlakani marehemu Muamar Ghadafi.Al-Saadi Gadhafi ameachiliwa huru baada ya kuwekwa kizuizini kwa zaidi ya miaka saba mjini Tripoli.
Kupitia ujumbe kwenye ukurasa wa Twitter, kaimu waziri Mkuu wa Libya Abdul Hamid Dbeibah ametangaza kuachiliwa huru kwa Al-Saadi kulingana na agizo la awali la mahakama.
Msemaji wa serikali ya mpito ya Libya Mohamed Hamouda amesema Al-Saadi aliondoka kwenye gereza la al-Hadaba, ambako maafisa wengi wa uliokuwa utawala wa zamani nchini humo wamefungwa.