Lowassa Ampongeza Rais Samia




Kwanza nianze kwa kumpongeza na kumshukuru Rais wetu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuifanya vyema kazi ya kuijenga nchi na kisha kuendeleza safari ya kujenga uchumi imara.

 

Kupitia hotuba yake katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, New York Marekani jana Alhamisi, Mama Samia amelirejesha tena taifa letu katika ramani ya dunia.

 

Katika kipindi kifupi alichokuwa madarakani, Rais Samia amefanikiwa kuanza kujenga imani ya sekta binafsi katika kushiriki kwenye ujenzi wa uchumi.

 

Safari ambayo hatuna budi sote kumuunga mkono na kumsaidia, ili aliwezeshe taifa kuwa imara zaidi kiuchumi na kuiweka nchi katika utawala wa sheria.

 

Rais Samia amethibitisha pasi na shaka kwamba Tanzania imepata nyota ya jaha kwa kuwa na kiongozi mkuu mwanamke hodari na shupavu ambaye leo hii tuna kila sababu ya kujivunia na kumuunga mkono.

Edward Ngoyai Lowassa
Waziri Mkuu wa zamani



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad