Machinga wa Arusha wameanza kuisoma namba baada ya kuambiwa kuwa hakuna tena vitambusho vya machinga hivyo wanatakiwa kulipa Tshs 500/= kila siku.
Wafanyabiashara hao hata walipoulizia kuwa mbona tuliambiwa tuwe na vitambulisho vya wamachinga vya Tsh 20,000/=?
Walijibiwa kuwa vitambulisho vya wamachinga vilizikwa Chato na kuanzia sasa wanatakiwa kutafuta TIN namba na kulipa ushuru kama wafanyabiashara wengine na kama wanataka kuwa wamachinga basi wabebe bidhaa zao na kuzunguka nazo si kukaa nazo sehemu moja …jambo hilo halipo kwa sasa.
Hata hivyo mbunge wa Arusha, Mrisho Gambo akiongea na wamachinga amesema kuwa akiwa bungeni Mh Waziri Mkuu alisema hadharani kuwa Serikali inavitambua vitambulisho vya wamachinga na wataviboresha na kuviweka picha ili viwe na sura na vimeshaanza kutolewa kwa elfu ishirini na mbunge huyo amesema wazi kuwa yeye yupo pamoja na wamachinga na hao wanaosema vitambulisho vimezikwa Chato basi ni wachonganishi na wanafiki.