Utaratibu wetu wa maisha unazunguka saa 24 kwa siku, na saa 12 za jua, na saa zingine zilizobakia ni wakati wa usiku. Lakini, je! Ulijua kwamba kuna maeneo ulimwenguni ambapo jua halizami kwa kwa zaidi ya siku 70?
Maeneo hayo ni haya hapa chini.
Norway
Norway, iliyoko kwenye mzunguko wa Aktiki, na huitwa ‘Ardhi ya Jua la Usiku wa Manane,’ ambapo kuanzia Mei hadi mwishoni wa Julai, jua halizama kabisa.
Hii inamaanisha kuwa kwa karibu kipindi cha siku 76, jua huwa halizami. Katika eneo la Svalbard, Norway, jua linaangaza mfululizo kutoka Aprili 10 hadi Agosti 23.
Pia ni mkoa wa kaskazini mwa Ulaya. Unaweza kupanga ziara yako mahali hapa wakati huu na kuishi kwa siku kadhaa, wakati kukiwa hakuna usiku.
Nunavut, Canada
Woman sitting on a balcony at sunset
Nunavut iko karibu digrii mbili juu ya mzunguko wa Aktiki, katika maeneo ya Kaskazini Magharibi mwa Canada.
Mahali hapa pana karibu miezi miwili ya jua kwa saa 24, huku wakati wa msimu wa baridi, mahali hapo huona karibu siku 30 mfululizo za giza kamili.
Iceland
Iceland ni kisiwa kikubwa zaidi barani Ulaya baada ya Uingereza, na pia inajulikana kwa kuwa nchi ambayo haina mbu. Wakati wa majira ya joto, usiku huwa uko wazi huko Iceland yaani hakuna giza, na wakati wa mwezi wa Juni, jua halizami kamwe.
Ili kuona Jua la usiku wa manane katika ubora wake likiwa linang’aa kweli, unaweza kutembelea jiji la Akureyri na Kisiwa cha Grimsey kwenye mzingo wa Aktiki.
Barrow, Alaska
A bright sun in an intensely orange sky
Kuanzia mwishoni mwa Mei hadi mwishoni mwa Julai, jua halizami hapa, ambalo baadaye hufidiwa kutoka mwanzoni mwa Novemba kwa siku 30 zijazo, ambapo jua halichomozi, na hujulikana kama usiku wa polar au ‘polar night’.
Hii inamaanisha pia kuwa nchi inabaki kwenye giza wakati wa msimu wa baridi kali. Eneo hilo pia ni maarufu kwa milima iliyofunikwa na theluji zenye kupendeza. Mahali hapa panaweza kutembelewa katika majira.
Finland
Ardhi yenye maelfu ya maziwa na visiwa, sehemu nyingi za Finland hupata kuona jua moja kwa moja kwa siku 73 tu wakati wa msimu wa joto. Wakati huu, jua linaendelea kuangaza kwa karibu siku 73, huku wakati wa msimu wa baridi, eneo hilo halioni mwanga wa jua.
Pia ni moja ya sababu kwanini watu hapa hulala kidogo tu wakati wa msimu wa jua, na zaidi wakati wa baridi. Ukiwa hapa, unafurahia Taa za Kaskazini na pia kupata fursa ya kushiriki mchezo wa kuteleza kwa ubao kwenye barafu.
Uswidi
Kuanzia mwanzoni mwa mwezi Mei hadi mwishoni mwa Agosti, Uswidi huona jua likitua karibu usiku wa manane na kuchomoza karibu saa 10 alfajiri. Hapa, kipindi cha jua kuwepo mara kwa mara kinaweza kudumu hadi miezi sita ya mwaka.
Kwa hivyo ukiwa hapa, mtu anaweza kutumia siku ndefu kwa kujishughulisha na kucheza gofu, uvuvi, kuchunguza njia za kusafiri, na mengine mengi zaidi.
Credit by BBC.