Magari ya serikali STK na STL yanayokwenda Mwendo Kasi na Kuvunja Sheria Barabarani Yatatembezewa Faini



JESHI la polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa ameweka bayana jumla ya madereva 44 wa magari ya serikali yaliyokamatwa katika operesheni ya kudhibiti makosa ya usalama barabarani wamechukuliwa hatua ya kisheria ikiwemo kulipa faini .

Aidha ametoa onyo , kwa madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani ikiwemo kwenda mwendo kasi na kusema wanaopita barabara kuu za mkoa huo wakaechonjonjo .

Wankyo alieleza na yale magari ya serikali STK,STL yanayokwenda mwendo kasi na kuvunja sheria za usalama barabarani nao watatembezewa faini bila uoga.

Akizungumzia suala hilo Wankyo ,alisema huu mkoa ni wa operesheni za kila kukicha ,maaskari wa usalama barabarani wapo kila kona kudhibiti makosa hayo pasipo kumuangalia mtu machoni .

Hata hivyo Wankyo ,alifafanua makosa ya usalama barabarani yalikamatwa 3,971 na yalilipiwa faini za papo kwa hapo ambapo zilikusanywa sh.milioni 119.130.

"Ukiwa katika barabara Kuu ya Morogoro ,ama Msata-Bagamoyo hautakiwi kuendesha unavyotaka wewe narudia sio wanavyotaka wao bali tunavyotaka sisi ,hii ni operesheni Mamba ,hatutomuacha mtu salama lazima tudhibiti makosa haya"

Wankyo pia alitoa rai kwa jamii kutoa ushirikiano wa kitaarifa za uhalifu wa aina yoyote kwa vyombo vingine ili wachukuliwe hatua za kisheria haraka.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad