Mahakama Yaifuta Kesi Iliyofunguliwa na Mbowe




MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, imeifuta kesi ya kikatiba Na.21/2021, iliyofunguliwa na kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini humo cha CHADEMA, Freeman Mbowe, kupinga utaratibu uliotumika kumkamata jijini Mwanza, kumuweka kizuizini na kumfungulia kesi ya ugaidi.

 

Kesi hiyo iliyokuwa inasikiliziwa na jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, wakiongozwa na Jaji John Mgetta, imefutwa leo Alhamisi, tarehe 23 Septemba 2021 na mahakama hiyo.

 

Kesi hiyo imefutwa kufuatia upande wa Jamhuri, kuweka mapingamizi manne juu ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Mbowe dhidi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG). Ukidai ni batili kwa kuwa ina upungufu wa kisheria.

 

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Mgetta amesema mahala sahihi kwa Mbowe kupeleka malalamiko yake ni Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam, ambako kesi inayomkabili inasikilizwa

“Kwa kuwa Mbowe analalamika tangu akamatwe Mwanza na kufunguliwa mashtaka haki zake za msingi zilivunjwa.”

 

“Kesi hii haiwezi kuendelea kwa kuwa Mbowe ana kesi nyingine, hii ni njia nyingine ya kuibua malalamiko yake,” amesema Jaji Mgetta

 

“Mahakama hii haitakuwa na mamlaka ya kuendelea na kesi hii wakati kesi nyingine inaendelea, Maombi haya nayafuta na kila mmoja abebe gharama zake,” amesema Jaji Mgetta.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad