Malkia Elizabeth aendelea kuwaombea waathiriwa wa shambulizi la 9/11





Malkia Elizabeth wa Uingereza amesema anaendelea kuwakumbuka na kuwombea waliopoteza maisha na manusura wa mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11 yaliyofanyika nchini Marekani mwaka 2001, huku akipongeza ushirikiano wa jamii katika kuijenga upya Marekani baada ya tukio hilo la kuogofya. 
Katika Ujumbe aliomtumia rais Joe Biden kwenye kumbukumbu ya miaka 20 ya mashambulizi hayo, Malkia amesema anaendelea kuliombea taifa la Marekani na familia zilizoathirika pamoja na wafanyakazi wa dharura waliokuwa kazini siku hiyo. 

Wakati huo huo rais wa Korea Kusini Moon Jae-in pia ametoa salamu zake za kumfariji rais wa Marekani Joe Biden na watu wa Marekani katika kumbukumbu hiyo ya miaka 20 tangu kutokea kwa mashambulizi hayo. 

Moon amesema Korea kusini kama mshirika muhimu wa Marekani itaendelea kusimama pamoja na taifa hilo katika vita vyake dhidi ya ugaidi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad