Mama Watoto wa Beka Flavor Ahusishwa Kutoka Kimapenzi na Patrick Kanumba


Muigizaji na Mfanya make up Happy Reuter mzazi mwenza na msanii Beka Flavour amedai sababu kubwa ya yeye na Beka kuachana ni kuigiza kwenye wimbo wa Ibraah unaoitwa "NIMPENDE" uliotoka miezi 7 iliyopita na si kingine.

Happy anadai akiwa location anafanya hiyo video alipigiwa simu na Beka kuwa hasirudi tena nyumbani aishie huko huko, kwa Mujibu wa Beka alidai wakati Happy anaenda kufanya hiyo Video hakuambiwa kuwa atakuwa Video Vixen bali aliaga kuwa anaenda kufanya Make up. Kitendo cha Happy kuwa Video Vixen kilimkwaza Beka na akaamua kumtimua.

Happy anadai hakuomba msamaha kwa sababu anamjua Beka ni mtu anayefanya maamuzi magumu na akiamua kufanya maamuzi huwa si mtu wa kuyabadilisha.

Wawili hawa waliwahi patanishwa kwenye kipindi cha LEO TENA cha Clouds Fm na kupewa tiketi za kuhudhuria show ya Mopao Koffi Olomide lakina haikuchukua muda kila mtu akafwata maisha yake.

Wakati wakipatanishwa Happy alitaka ndoa ili awe mke halali wa Beka maana anaishi naye bila kuwa na ndoa na ni kurisk maisha yake kwani siku Beka akiamua kumtimua anamtimua tu.

Pia Happy amekiri kuwa Beka anahudumia mwanaye kwa 100% bila tatizo lolote na kwasasa mwanadada huyu anahusishwa kuwa kwenye mahusiano na Othman Njaidi (Patrick Kanumba).

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad