Mama yake Ronaldo Alivyotokwa na ‘Chozi’ la Furaha




Mama yake mzazi na mchezaji bora kabisa duniani, Cristiano Ronaldo mwishoni mwa juma alishindwa kuzuia hisia zake na kujikuta akibubujikwa na machozi mbele ya kadamnasi pale alipomshuhudia mtoto wake akicheka na nyavu mara mbili kwenye mchezo wake wa kwanza dhidi ya mabosi wake wapya Manchester United.



Ronaldo mwenye umri wa miaka 36, alitupia magoli hayo mawili kwenye ushindi wa 4 – 1 mbele ya Newcastle.

Picha inayomuonyesha mama huyo mwenye umri wa miaka 66 akimwaga machozi alipokuwa Old Trafford imepata umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii.



Mwanadada aliyefahamika kwa jina Ambo_91 aliposti picha hiyo kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter na ndani ya muda mchache ‘tweet’ hiyo ilipata zaidi ya like 20,000 na karibia ‘retweet’ 4,000.

Uwepo wake uwanjani ulikuwa kama ‘surprise’ kwa Ronaldo ambaye aliwahi kusema kuwa mama yake aruhusiwi kwenda uwanjani kumuangalia hasa kwenye mechi kubwa.

”Kwa sasa aruhusiwi kuja kuangalia mechi kubwa,” Ronaldo amemwabia mwandishi wa habari, Piers Morgan.

”Sina baba tena, sihitaji kumpoteza na mama pia, hutaweza kuangalia robo fainali, nusu fainali au fainali,” – Ronaldo amesema alichomuambia mama yake.

Imeandikwa na @fumo255

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad