Manchester United yachezea Kipigo Huku Ronaldo Akifunga Bao Moja


PAMOJA na kufunga, lakini Cristiano Ronaldo hakuiepusha timu yake, Manchester United na kipigo cha 2-1 kutoka kwa wenyeji, Young Boys katika mchezo wa Kundi F Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Wankdorf Jijini Bern,

Ronaldo alianza kuifungia Manchester United dakika ya the 13 akimalizia krosi ya Mreno mwenzake, Bruno Fernandes kabla ya Aaron Wan-Bissaka kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 35 kwa kumchezea rafu, Christopher Martins.

Baada ya hapo Young Boys wakauteka mchezo na kupata mabao yao mawili kupitia kwa Moumi Ngameleu dakika ya 66 na Jordan Siebatcheu dakika ya 90 na ushei akitumia makosa ya Jesse Lingard aliyechukua nafasi ya Ronaldo dakika ya 72 kutoa pasi butu ya nyuma.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad